Shirika la Bima la Taifa (NIC) limekuwa likishiriki maonesho mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu na huduma za bima kwa wananchi ili kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za bima nchini.
Kwenye Maonesho ya 12 ya Kimataifa Zanzibar (ZITF 2025) yanayoendelea visiwani humo yamewezesha NIC kunadi chapa yake yenye zaidi ya miaka 63 katika sekta ya bima ikiwahakikishia wadau huduma bora za bima zenye viwango vya kimataifa kama inavyotambulika kimataifa (ISO Certified).
NIC ni kampuni kiongozi kwenye sekta ya bima kwa kutoa huduma bora za bima za mali na ajali kwa zaidi ya miaka 63 sasa.
#sisindiyobima #niczif2025