Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Bw. (Jina kamili), ametembelea banda la NIC katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita.
Katika ziara hiyo, Meneja huyo alipokea maelezo ya kina kutoka kwa maafisa wa NIC kuhusu namna taasisi hiyo ya bima ya umma inavyoshiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya bima na huduma za kifedha kwa wananchi na wadau wa sekta ya madini.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na maafisa wa NIC, ushiriki wao katika maonesho haya ni sehemu ya mpango mpana wa taasisi hiyo wa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa bima katika kulinda maisha na mali za wananchi hasa katika sekta ya madini inayokua kwa kasi nchini.
“NIC imeendelea kuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya bima kupitia majukwaa mbalimbali, ikiwemo maonesho ya kitaifa kama haya na pia kupitia kampeni maalum ya ‘NIC Kitaa’ inayofanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani,” alieleza Juve…..
Elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa bima kama nyenzo ya kupunguza athari za majanga, kuongeza uaminifu wa wawekezaji, na kuchochea ustawi wa kiuchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Maonesho ya Teknolojia ya Madini Geita ni jukwaa muhimu la kuwakutanisha wadau wa sekta ya madini, teknolojia, fedha, na bima, na mwaka huu yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
⸻
Banda lipo mkabala na REA/TANESCO na TTC, Geita
#NICInsurance
#SisIndiyoBima
#TIRA
#MadiniGeita2025
#BimaKwaMaendeleo