Success, we'll get back to you
Back to news

RC Dodoma apongeza NIC kwa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa huduma za bima

SHARE

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ameipongeza Shirika la Bima la Taifa (@nic_insurance ) kwa juhudi zake za kuwaunganisha wananchi pamoja na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa huduma za bima ili kujikinga na majanga mbalimbali.


Mhe. Senyamule ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na NIC na kufanyika katika ukumbi wa New Generation jijini Dodoma, ambapo aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kujifunza na kuchangamkia huduma za bima kwa ajili ya kulinda maisha na mali zao.


Amesema utoaji wa elimu kuhusu bima kwa jamii ni muhimu kwani unasaidia wananchi kuelewa namna ya kukabiliana na athari za majanga yanayoweza kutokea bila kutarajia.


Awali, Meneja wa Biashara na Usimamizi wa Mawakala kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Nicklous, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo, alisema kuwa kukutana pamoja katika Iftar ni fursa ya kuimarisha ukaribu kati ya taasisi, wadau na wananchi.


Alisema NIC itaendelea kuboresha huduma zake za bima ili kuwasaidia wananchi kujilinda na majanga mbalimbali kama moto, mvua kubwa na matukio mengine yasiyotarajiwa, huku akiwahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kukata bima kwa ajili ya usalama wa maisha na mali zao

@2026

National Insurance Corporation of Tanzania Limited