NIC kwa kushirikiana na banki ya NMB kwa pamoja tumezindua kampeni ya UMEBIMA iliyolenga kufikisha huduma za bima kwa wananchi mtaani kupitia njia za kidigitali ambazo zitamuwezesha mwananchi kukata bima kupitia simu ya janja (WhatsApp na Aplikesheni ya NIC Kiganjani). Uzinduzi wa kampeni umefanyika Makao Makuu ya NMB.
Uzinduzi huu umefanywa na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Ndugu Karimu Meshack kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Ndg. Kaimu Abdi Mkeyenge na Mkuu wa Idara ya Bima wa NMB, Ndg. Martine Massawe.
Karimu Meshack amesema “Ushirikiano huu wa NIC na NMB utasaidia kuongeza kasi ya uelewa wa Bima kwa wananchi kwa kuzingatia njia rahisi ya kukata bima tuliyoiweka, hapa ni mwendo wa kidijitali tu”
Kwasasa wateja wa NIC wanaweza kukata bima kupitia NMB JIRANI kwa njia ya WhatsApp kwa namba 0747 333 444 kwa kuchagua NIC au kupitia NIC Rafiki kwa njia ya WhatsApp kwa namba 0684 598 912.
#nicinsurance #sisindiyobima