Success, we'll get back to you
Back to news

NIC Yaendelea Kutoa Elimu na Huduma za Bima Katika Kijiji cha Bima – Geita 2025.

SHARE

Geita, Tanzania 


NIC inaendelea kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu na huduma za bima kwa wananchi kupitia Kijiji cha Bima kilichoko kwenye Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.


Kijiji cha Bima ni mkusanyiko wa watoa huduma mbalimbali wa bima nchini, waliounganishwa chini ya uratibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) [@tira_tz], kwa lengo la kutoa elimu, ushauri na huduma za bima kwa wananchi na wadau wa sekta ya madini na biashara.


NIC, kama taasisi ya umma inayojikita katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa bima, inatoa huduma za:

✅ Bima ya maisha

✅ Bima ya mali

✅ Bima kwa wachimbaji

✅ Ushauri juu ya aina sahihi za bima kwa mazingira mbalimbali ya kibiashara na kijamii


“Ushiriki wetu katika Kijiji cha Bima ni sehemu ya dhamira ya NIC ya kuendelea kufikisha elimu ya bima kwa wananchi kwa njia rahisi na ya moja kwa moja, tukishirikiana na mamlaka na taasisi nyingine,” alisema Ephrasia Mawala, Afisa Uhusiano wa NIC.


Maonesho haya ni fursa muhimu ya kuwasogezea wananchi elimu ya kifedha, hasa kupitia bima, ambayo ni nyenzo ya msingi ya kujikinga na athari za kiuchumi zitokanazo na majanga mbalimbali.


Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la TIRA – Kijiji cha Bima, ili kupata huduma na maelezo kutoka kwa NIC pamoja na watoa huduma wengine wa bima waliopewa kibali cha kutoa huduma chini ya usimamizi wa TIRA.



Geita – Banda la TIRA, Kijiji cha Bima

NIC – Sis ndiyo Bima ya Taifa.


#NICInsurance

#SisIndiyoBima

#TIRATanzania

#KijijiChaBima

#MadiniGeita2025

@2025

National Insurance Corporation of Tanzania Limited