Katika jitihada za kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kuongeza ukaribu na wateja wake, Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeendelea kushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC, Bw. Karimu Meshack, ametembelea mabanda ya taasisi mbalimbali za kifedha, bima na madini ikiwa ni pamoja na NMB Bank, Equity Bank, Bluecoast, PSSSF, NSSF, NHIF, Kampuni ya Madini ya FEMA, pamoja na HEXAD Insurance Agency.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika banda la NMB, Bw. Meshack alisema:
“Tumekuja kuwashukuru kwa kuendelea kutumia huduma za bima kutoka NIC. Pia tunalenga kuimarisha uhusiano wetu wa kibiashara, kutambua changamoto zilizopo na kuhakikisha tunazitatua kwa wakati.”
Maonesho haya ni jukwaa muhimu linalowakutanisha wadau kutoka sekta ya madini, teknolojia, fedha na bima. Kwa mwaka huu, yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).
NIC inaendelea kuwakaribisha wadau wote kutembelea banda lake lililopo karibu na mabanda ya REA/TANESCO na TTC, kwa ajili ya kupata elimu kuhusu huduma za bima, ushauri wa kitaalamu na huduma nyingine mbalimbali.
ttps://www.linkedin.com/posts/nic-insurance-7b3b021b9_nic-yatembelea-wateja-na-wadau-katika-maonesho-activity-7377685579469127680-T4hF?utm_source=share&utm_medium=member_desktop&rcm=ACoAADLjJfcBbUk-dTC7StAkCE6hhu2420DDKHE