Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea banda la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) na amepokelewa na Afisa Uhusiano Bi. Ephrasia Mawalla kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge.
Mhe. Dkt. Jakaya amefurahishwa na huduma za bima za maisha (BeamLife) mara baada ya kupatiwa maelezo ya kina na Afisa Bima Bi. Thecla Mtege.
Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yamehitimishwa leo Julai 13, 2025 na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa