Success, we'll get back to you
Back to news

NIC Yatoa Elimu Ya Bima Kwa Waalimu Na Wanafunzi Wa Sekondari Jijini Mwanza.

SHARE

NIC Insurance imetua katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Musabe mkoani Mwanza kwa ajili ya kutoa elimu ya Bima kwa Waalimu na Wanafunzi wa shule hiyo.


Akizungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo kabla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Uandishi wa Insha Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance Karimu Meshack amesema kuwa NIC imeamua kuanzisha Klabu ya Bima ya wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi Musabe.


Amesema kuwa watoto ndio Taifa la leo na kesho, wakifundishwa na kuelewa Bima, Taifa zima litajua umuhimu wa Bima.


Hata hivyo katika mashindano hayo NIC ilitoa zawadi ambazo ni iPad, mabegi, t-shirts na cheti kwa washidi wa 01 hadi 10.


Meshack amesema kuwa suala la bima uelewa wake ni asilimia ndogo sana hivyo ni lazima kuiongeza ili kwenda na malengo ya serikali ambayo ni kufikia asilimia 50.


Amesema kuwa wanatoa elimu ya bima ya maisha pamojà na bima ya Mali na Ajali huku wakiamini wanafunzi ndio daraja la kwenda kuongeza uelewa wa bima kwa watanzania.


Aidha amesema kuwa watu wakipata majanga wanaishia kulia hali ambayo inakua imesababushwa na kutokuwa na bima.


Amesema wataendelea kutoa elimu ya Bima kwa kutumia majukwaa mbalimbali wakiwemo wanafunzi ambao amewapa ubalozi wa NIC Insurance na Bima kwa ujumla.


Nae Makamu Mkurugenzi wa Shule za Musabe Faustine Magabilo amesema kuwa anaishukuru NIC Insurance kwa kuichagua Shule hiyo kwa wanafunzi kushiriki uandishi wa Insha na kunafanya Shule kuweka kumbukumbu isiofutika.


Amesema kuwa kama Taasisi wana majengo na magari ambapo kutokana na elimu hiyo ni wakati wao kuwa mabalozi kutokana na elimu ya bima walioipata.


Magabilo amesema kuwa anawapongeza wanafunzi kuwa na utayari na kushiriki ipasavyo na kupatikana washindi hali hiyo inaonyesha kwenda kuwa mabalozi na hata ambao hawajakuwa washindi waamini wameshinda kwani kulikuwa hakuna kundi la kufeli.

@2024

National Insurance Corporation of Tanzania Limited