Morogoro. Baraza la Wafanyakazi la Shirika la Bima la Taifa (NIC) limekutana mkoani Morogoro kujadili maendeleo ya shirika, ustawi wa wafanyakazi na mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma za bima kwa wananchi.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Bwana Kaimu Abdi Mkeyenge, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza, Abdul Karim Kisuguru, alisema lengo la mkutano huo ni kuimarisha utendaji wa shirika na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma.
Kisuguru alibainisha kuwa majadiliano hayo ni sehemu ya mpango mpana wa NIC wa kuendelea kuboresha mazingira ya kazi, kuongeza motisha kwa wafanyakazi na kuimarisha ushindani wa shirika katika soko la bima nchini.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Menejimenti ya Shirika, Wawakilishi wa Wafanyakazi, Wawakilishi kutoka Ofisi ya Kamishna wa Kazi pamoja na Chama cha Wafanyakazi Tanzania. Washiriki walijadili changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta ya bima na kuweka mikakati ya kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na NIC.
Baraza hilo limeahidi kutekeleza maazimio yaliyofikiwa ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora, kuongeza tija na kuendelea kujenga uhusiano mzuri kati ya menejimenti na wafanyakazi.
#SisiNdiyoBima