Katika mkakati wa kutoa huduma bora za bima kwa wananchi, NIC imeendelea kutoa mafunzo kwa Watumishi ili kuwaongezea ujuzi wa namna ya kutoa huduma bora kupitia bidhaa zake za bima za Maisha.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayoendelea kufanyika mjini Morogoro, yamelenga kuongeza ujuzi na namna bora ya kutoa huduma za bima za maisha kwa wateja.
Kaimu Mkurugenzi wa Bima za Maisha Bw. Petro Mgaya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, katika ufunguzi wa mafunzo hayo amesisitiza umuhimu wa mafunzo ni kushirikishana uzoefu wa namna bora ya kuwahudumia wateja kwa kuzingatia mkataba wa bima na kutambua ushindani wa soko uliopo Nchini.
#NICBima #BimaKwaWote #TunajaliUlinziWako